SIKU chache baada ya Meya wa Manispaa ya Ilemela Henry Matata
kutishia kumuua Mbunge wa Jimbo la Ilemela Highanes Kiwia (Chadema),
Mbunge huyo ameitisha maandamano makubwa ya wananchi kutaka meya aondoke
madarakani akidai a hakuchaguliwa halali.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Magomeni jijini hapa, Mbunge Kiwia alisema maandamano hayo yanatarajiwa kufanyika Alhamisi ijayo.
Kiwia alisema wananchi watapiga kambi katika ofisi za Halmashauri ya Manispaa katika jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela eneo la Buswelu.
Alisema lengo la maandamano hayo ni kuhakikisha neya huyo anaondoka madarakani kwa kuwa hakuchaguliwa halali akidai sheria na kanuni zilipindishwa kwa lengo la kumbeba.
Meya huyo, Matata alifukuzwa na Chadema na hivi sasa suala lake liko mahakamani.
Mbunge huyo aliwataka wananchi wajitokeze kwa wingi katika maandamano hayo ambayo ameyaelezea kuwa ni ya aina yake yenye kulenga kutetea haki za wananchi.
Aliwataka wananchi wasiogope kujitokeza kwa kuwa maandamano ni haki yao katika sheria.
Kiwia alidai Chadema pamoja na wananchi wa Ilemela hawamtambui Matata ambaye ni diwani wa kata ya Kitangiri kuwa ni Meya wa Ilemela.
Alidai Matata alichaguliwa kinyemela na madiwani sita pekee kati ya madiwani 14 wanaounda Manispaa ya Ilemela.
“Nawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi katika maandamano hayo ambayo yataishia katika ofisi za halmashauri ya Ilemela.
“Bahati nzuri hata wenzetu wa Nyamagana wamekubali kutuunga mkono katika harakati zetu za kumng’oa Matata kama meya.
“Mnapaswa kuchukua chakula cha kutosha na ni lazima tupiganie haki yetu kwa amani,” alisema Kiwia.
CHANZO GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment