Mkurugenzi wa Stopper Entertainment, Mursin Mambo, akifafanua jambo kuhusiana na Mashindano ya Shule za Sekondari.
Mashindano ya Mijadala kwa shule za sekondari mkoani Mwanza
(Interschools Debate Competition), yanatarajiwa kuanza septemba 02 mwaka
huu.
Akizungumza
katika semina elekezi, iliyowakutanisha baadhi ya walimu wa mijadala
kutoka katika shule mbalimbali za sekondari mkoani Mwanza, mkurugenzi
wa Stoppers Entertainment ambao ndio waandaji wa shindano hilo, Bwana
Mukhsin Mambo, amesema jumla ya shule 32 kutoka mkoani Mwanza,
zitashiriki katika shindano hilo ambalo ni la kwanza kufanyika mkoani
humo na Tanzania kwa ujumla.
Mambo,
amesema shindano hilo pia litaonyeshwa kwenye moja ya runinga hapa
nchini kuwapa fursa watazamaji kushuhudia vipaji vya wanafunzi katika
kujieleza mbele ya jamii.
Amesema
nia na madhumuni ya shjindano hilo, mbali na kuondoka na kitita cha
zawadi kwa washindi lakini pia ni njia mojawapo ya kuinua kiwango cha
elimu hapa nchini kwa wanafunzi kupata nafasi ya kujieleza mbele za
watu, kufanya utafiti kutokana na mada itakayowekwa mezani, kuweka
mahusiano mema dhidi ya wanafunzi na kujenga kizazi kipya katika nyanja
ya elimu kupitia mfumo wa mijadala.
Miongoni
mwa shule zitakazoshiriki shindano hilo ni pamojana Nsumba sekondari,
Nganza Sekondari, Butimba sekondari, St. Joseph Girls Sekondari, Buswelu
Sekondari, New Hellen Sekondari, Hill crest Sekondari, Bismark
Sekondari.
FATHER KIDEVU BLOG
0 comments:
Post a Comment