Wasanii
Raymond Kigosi na Steven nyerere wakiwafurahisha washabiki wao kwenye
uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival
jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na
kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji
cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza
Wasanii
wakibadilishana mawazo na baadhi ya wasanii chipukizi wa jiji la Mwanza
kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim
Festival jijini Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu
nchini na kuanza jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa
kinywaji cha Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza.
Wananchi
mbalimbali wa jiji la Mwanza wakishangilia kwa nguvu kwenye uzinduzi wa
Tamasha la filamu la Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini
Mwanza ambalo liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza
jana kwenye kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha
Grandmalt na Isamilo Lodge ya Mwanza
Wasanii
wakiwa katika picha ya pamoja kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la
Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo
liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye
kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na
Isamilo Lodge ya Mwanza
mashabiki
wakiwa katika nyuso za furaha kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu la
Grandmalt Tanzania Open Fillim Festival jijini Mwanza ambalo
liliwashirikisha wasanii wote wa filamu nchini na kuanza jana kwenye
kiwanja cha Nyamagana chini ya udhamini wa kinywaji cha Grandmalt na
Isamilo Lodge ya Mwanza.
======== ====== ======== ===========
Uzinduzi Tamasha la Filamu Grand Malt lawakuna wakazi wa jiji la mwanza
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WAKAZI
wa Mwanza na vitongoji vyake juzi walishuhudia vitu tofauti wakati wa
uzinduzi wa Tamasha la Filamu la Wazi la Granda Malt Tanzania,
ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, lililofanyika
kwenye Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa.
Tamasha
hilo maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lilinogeshwa
zaidi na burudani kali kutoka kwa bendi ya Extra Bongo, waliokuwa
wakiongozwa na Ally Choki.
Shamrashamra
za uzinduzi huo zilionekana toka mapema alfajiri, wakati wasanii wa
Bongo Movie walipojikuta wakibanwa kila mahali walipokuwa wakipita
kutambulisha ujio wao.
Wakati
wa uzinduzi huo, wasanii waliokuwepo uwanjani hapo wakiongozwa na
Hashima Kambi, walijikuta wakizongwa kwa muda wote, huku mashabiki
wakitaka kuwashika au kupiga nao picha.
Aunty
Ezekiel, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Jacob
Steven ‘JB’ walijikuta wakishangiliwa muda wote kama ilivyokuwa kwa
Hashim Kambi, Isa Musa ‘Cloud’ na Steve Nyerere.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya,
alisema amefurahishwa mno na tamasha hilo na hasa watu waliokuwa
wamejitokeza kwa wingi kushuhudia wasanii wao.
“Serikali
itaendelea kuthamini kwa kiasi kikubwa wasanii wetu na huu ni wakati wa
wasanii wa Mwanza kujifunza kutoka kwa mastaa wetu hawa,” alisema.
Meneja
wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema, wameamua
kulidhamini tamasha hilo kwani wanajua watu wengi kwa sasa wanapenda
kutazama filamu za Tanzania.
“Pia
tunapenda kuwashauri muendelee kutumia kinywaji cha Grand Malt ambacho
hakina kilevi, badala ya kumpa mtoto vinywaji ambavyo manufaa unaweza
pia kumfungashia kinywaji hiki katika matumizi yake,’ alisema.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema wamefurahishwa mno na
mapokezi waliyoyapata na hawakutarajia kukutana na mashabiki
waliowakubali kama hao.
“Nimefurahishwa
mno na hiki kitu, kusema kweli Mwanza tutaendelea kupakumbuka,” alisema
JB akiungwa mkono na Ray, huku Wolper akidai lazima atarejea tena. Mratibu
wa Tamasha hilo aliye pia Mkurugenzi wa Sophia Records, Musa Kissoky,
alisema tamasha hilo litaendelea kwa muda wa wiki moja ambapo filamu
mbalimbali zitaonyeshwa.
Kissoky
alisema, tamasha hilo ambalo ni la bure kwa watu wote na kushirikisha
mastaa wa filamu hapa nchini, litakuwa la aina yake kwani vitu
vitakavyofanyika vitakuwa si vya kawaida.
Tamasha
la Filamu la Grand Malt limeanza rasmi juzi na litamalizika mwishoni
mwa wiki huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi
hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.
Tamasha
hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na
kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL) na Isamilo Lodge na Club Lips zote za jiji la Mwanza
0 comments:
Post a Comment