MKURUGENZI wa Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Luteni
Jenerali Sylivester Ryoba amewashukia wabunge kwa kujitwisha majukumu ya
kusimamia maafa yanapotokea katika maeneo yao kwa lengo la kusaka sifa
kwa wapiga kura wao, badala ya jukumu hilo kufanywa na kamati za maafa
zilizopo.
Ryoba aliyasema hayo katika mkutano wa kutoa mafunzo ya namna ya kupambana na kukabiliana na majanga Mkoa wa Mwanza, pamoja na wilaya zake jijini hapa.
Mkurugenzi huyo alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakitekeleza majukumu ambayo si yao wakati wa majanga na maafa yanapotokea katika maeneo yao na wakati mwingine kutaka kulazimisha kusimamia hata ugawaji wa chakula na vitu vingine.
“Kuna baadhi ya wabunge wamekuwa wakichukua majukumu ambayo sio yao katika matukio mbalimbali, kwa lengo la kutaka kuonekana wapo. Wao ni wawakilishi wa wananchi hatuwakatazi lakini kuna mipaka yao, wamekuwa wakijichukulia majukumu ambayo si yao.
“Siwasemi vibaya wabunge kwa kuwa hawapo hapa, lakini kwa kuwa kuna wawakilishi wao naomba wawafikishie salamu hizi na wamekuwa wakipiga kelele sana, napenda kuwafahamisha kuwa waziheshimu kamati za maafa zilizopo kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa ofisi yake imeamua kutoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na majanga na maafa kabla na baada kwa kamati za mikoa yote na wilaya Tanzania bara.
Alisema kuwa mafunzo hayo yanapaswa kufikishwa hadi katika ngazi za vijiji, ili kuwafikishia wananchi mbinu mbalimbali ambazo wanapashwa kuzichukua pindi wanapofikwa na majanga na maafa.
Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga alisema halmashauri katika mkoa huo zinapaswa kutumia sheria za mipango miji zilizopo kwa ajili ya kuzuia wananchi kuishi katika maeneo ambayo ni hatarishi hususani mabondeni.
CHANZO GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment