SERIKALI
imesema haitachukua dhamana kwa mtu atayeadhirika kiafya kwa kuvamia kisha
kujenga makazi kwenye hifadhi ya Mlima wa Kiseke katika manispaa ya Ilemela
mkoani Mwanza kutokana na eneo hilo kutengwa kwa ajili ya kujenga kituo cha
Rada ya Hali ya hewa.
Kauli hiyo imetolewa na
Naibu waziri wa Uchukuzi,Dk. Charles Tizeba wakti akizundua mradi wa kufikisha
taarifza za hali ya hewa kwa wakulima,wafugaji,wavuvi na wasafirishaji katika
Bonde la ziwa Victoria uliowekwa katika kijiji cha Nykarilo wilayani Sengerema.
Amesema Rada hizo hutoa
Mionzi hatari ambayo huleta madhara makubwa kwa Afya za Binadamu Kama ugonjwa
wa kansa na watoto kuzaliwa wakiwa walemavu.
Kauli hiyo ilikuja
kufuatia eneo hilo kuvamiwa na watu kisha kujenga makazi ya kuishi hatua ambayo
inaweza kuwaletea madahara ya kiafya inayotokana na Rada hiyo.
Kutokana na kuwepo kwa
uvamizi huo,Dk.Tizeba amewataka watumishi wa Ardhi na mkuu wa wilaya ya
Ilemela,Amina Masenza kuhakikisha wanadhibiti uvamizi huo.
Aidha mkurugenzi mkuu wa
mamlaka ya hali ya hewa nchini,Agnes Kijazi amesema mradi huo wa majaribio wa
majaribio umegharimu dolla 160,000 kwa ufadhili wa kutoka nchi ya Norway na
kwamba utasaidia kukabiliana na maafa yanayotokana na mvua,upepo ziwani kupitia
utaratibu maalumu kwa kushirikiana na taasisi na mamlaka zilizopo.
0 comments:
Post a Comment