WATU wawili wamepoteza maisha katika wilaya ya Ukerewe, Mwanza katika matukio mawili tofauti likiwemo la mwanafunzi wa shule msingi Nantare kuuawa na Mamba.
Matukio hayo hasa la mwanafunzi kuuawa na Mamba yametokea kwa nyakati tofauti katika kata ya Ngoma inayokabiliwa na changamoto nyingi zinazosababishwa na wanyama pori
Afisa mtendaji wa kata hiyo Khamis Ndaro amewataja watu walipoteza maisha kuwa Paschal Adudalla [14] mwanafunzi wa shule ya msingi Nantare aliyepatwa na mauti hayo majira ya saa. 1. 30 usiku juma tano wiki hii na mwili wake ulipatikana siku iliyofuta ukiwa na majeraa
Katika tukio lingine lililotokea majira ya saa. 12.30 alfajili juzi katika kijiji cha Hamkoko katani hapo Mtu mwingine Mtimba Manyenye [64] alipigwa na Radi akiwa shambani kwake na kupoteza maisha hapo hapo.
Mdogo wake na marehemu Paschal aitwae Paul Sostenet [14] pia mwanafunzi wa shule hiyo aliyeshuudia sakata hilo amesema kaka yake alikamatwa na kuchuku na mnyama huyo baada ya kuingia katika ziwa Victoria kuoga muda mfupi walipokamisha shughuri ya kumwagilia bustani yao ya Nyanya.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Hamkoko walioshuudia mwili wa mtu aliyepigwa na Radi wamesema ngozi ya mwili wake ilikuwa sawa na mtu aliyeungua moto pamoja na nguo zake.
Akieleza adha ya wanyapori katani hapo Ndaro alisema mtu mwingine aitwae Domician Bagaile [ 32] amepoteza kidole cha mkono wa kushoto hivi karibu wakati aliposhambuliwa na Mamba akiwa kando kando ya ziwa akivua samaki kwa ndoano.
Katika hatua nyingine afisa mtendaji huyo wa kaya ya Ngoma amesema wanyama pori wengine aina ya Nyani zaidi ya 1,000 pamoja na Viboko wamesababisha Ekali zaidi ya 150 za mashamba ya wakulima kutolimwa msimu huu wa kilimo
Alisema wakulima wamekata tamaa kulima mashamba yao msimu huu wa kilimo kwa hofu ya mazao yao kualibiwa na wanyama hao ambao kwa miaka kadhaa ualibu mazao yao ya aina mbali mbali ikiwemo mahindi , mpunga na viazi vitamu hasa katika vijiji viwili vya Muluseni na Nantare.
Hata hivyo amesema pamoja na maafisa wanyapori kuendesha misako ya mara kwa mara , wanyama hao wanaendelea kuwa tishio hasa Nyani ambao ujificha katika vilima vyenye mapango na baada ya muda ujitokeza na kualibu mazao.
Afisa idara ya maliasili na mazingira wa halmashauri ya wilaya Joseph Song’ola amekili kuwa matukio hayo hasa utokea wakati wa msimu wa kilimo ambapo wakazi wa vijiji vinavyopakana na ziwa Victoria uvamia na kulima maeneo ya ifadhi ya ziwa hilo wakati wakielewa eneo la ndani ya mita 600 limetengwa kwa ifadhi na malisho ya wanyama hao.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment