Mwandishi wetu, Mwanza
Serikali imesema itaongeza mishahara na vitendea kazi kwa askari wa wanyamapori ili kuongeza motisha kwa akari hao katika kupambana na ujangili katika hifadhi za taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu wakati akizungumza na watumishi wa Chuo cha Wanyama Pori mjini Mwanza
Nyarandu aliwataka wadau wote wa utalii na mali asili nchini kutumia ubunifu na fikra chanya katika kuleta mabadiliko katika sekta hizo badala ya kufikiria kuwa haiwezekani.
Amesema kuwa endapo wadau hao watazingatia utumiaji wa fikra walizonazo kubadili mifumo na sera zinazokwamisha ukuaji wa sekta ya utalii na maliasili kwa kuzingatia uzalendo ni dhahili maendeleo yatonekana
Amfeafafanua kuwa ubunifu katika kutangaza vivutio vya utalii kwa kuwa na kauli mbiu zisizobagua maeneo yanayovutia nchi nzima na kubadili mitaala ya ulinzi kwa kutumia mbinu mpya ikiwemo intelijensia katika kutaboresha utalii nchini.
Hata hivyo alisema kuwa kuwafundisha wanafunzi wa hifadhi za taifa bila kuwaajili kwa muda mrefu ni hatari kwani wanaweza kutumiwa na baadhi ya watu wenye nia mbaya katika ujangili.
Alishauri kubadili mitaala kwa kufundisha mbinu za kijeshi na kuongeza mbinu za kiintelejensia ili kurahisisha kuwabaini na kuwazuia majangiri kabla ya kuvamia hifadhi hizo.
Aidha amekemea mfumo wa baadhi ya watu katika sekta ya utalii kuweka ukiritimba katika leseni za uwekezaji kwani kunanufaisha watu wachache jambo lisilo la haki.
Pia aliwataka wataalam wa utalii na wanyamapori kutafuta maarifa wenyewe badala ya kusubiri kwenda kwa wataalamu wengine jambo linaloongeza gharama.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment