Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu amewaagiza Wakurugenzi wa Idara ya Wanyapori Nchini kuhakikisha wanaandaa mapendekezo ya sheria ya mamlaka ya wanyamapori
Alisema kuwa mapendekezo hayo yanapaswa kuandandaliwa mapema na kufikishwa wizarani ili kupelekwa bungeni kama mswada ikiwa ni harakati za kuboresha sekta hiyo ambayo ni muhimu katika maendeleo ya taifa.
Akizungumza na Wkurugenzi wa Wanyama Pori Mkoani Mwanza, Nyarandu alishauri idara kuangaklia utaratibu wa kujitegemea kama ilivyo kwa TANAPA ili kupata mapato yake yenyewe badala ya kutegemea kutoka serikali kuu.
Pia Waziri nyarandu alisema kuwa kuna tetesi za kuwepo baadi ya watendaji wachache wasio waaminifu wanaoshirikiana na majangili kuhujumu nyara za serikali jambo ambalo lazima likomeshwe.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment