Mwandishi wetu, Mwanza
Zoezi la upimaji wa maeneo ya wananchi na uuzaji wa viwanja unaofanywa na halmashauri ya jiji la wanza limesababisha makampuni binafsi kubuni mbinu za kupima maeneo ya wananchi na kuyauza holela.
Hali hiyo imebaini katika eneo la lukobe kata ya ilemela wilayani ilemela mkoani mwanza, kampuni ya JULMART imepima maeneo ya wananchi na kutoa jumla ya viwanja 900.
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wetu umebaini kuwa kati ya viwanja vitano kwa viwanja 900, viwili vinachukuliwa na kampuni hiyo na kuuzwa kati ya shilingi 1, 500,000 na shilingi 2,000,000.
Mkurugenzi wa kampuni ya JULMART Martine Masawe amesema kuwa zoezi la upimaji wa maeneo ya wananchi na kuyauza limeanza tangu mwaka mmoja na nusu uliopita baada Ya kupata kibali kutoka halmashauri ya jiji la mwanza.
Amesema kuwa zoezi hilo wamelifanya katika eneo la Nyamhongoro ambapo wamepima viwanja 100 na kuviuza , eneo la kahama wamepima viwanja 70 na eneo la lukobe wamepima viwanja 900 ambavyo baadhi ya viwanja hivyo wameanza Kuviuza.
Hata hivyo baadhi ya wananchi wa maeneo ya lukobe wamesema kuwa walilazimika kuruhusu upimaji na kutoa viwanja vyao baada ya kampuni hiyo kuahidi kutoa hati kwa wananchi hao jambo ambalo halijatekelezeka.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment