Na Christopher Gamaina, Mwanza
DIWANI wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata (Chadema), ametangaza nia ya kugombea nafasi ya umeya wa Manispaa ya Ilemela. Hata hivyo, Matata ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji, Ujenzi na Mazingira jijini Mwanza, anategemea baraka za chama chake kugombea kiti hicho.
Hivi karibuni, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), ilikubali ombi la kuigawa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa kuanzisha Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela itakayojitegemea.
Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa juzi, Matata, alisema haoni sababu ya kutojitupa katika kinyang’anyiro cha umeya wa Manispaa ya Ilemela, kwa kuwa hiyo ni mojawapo ya hatua za kukitendea haki chama chake.
“Unajua ukishaingia katika chama cha siasa lazima ukitendee haki ambayo ni pamoja na kugombea uongozi. Lakini pamoja na jina langu kutajwatajwa lazima nipate baraka za chama changu niweze kugombea umeya wa Ilemela,” alisema Matata.
Alisema Manispaa mpya ya Ilemela inahitaji mtu mwenye ushawishi mkubwa wa kisiasa, uhusiano na jamii, msimamo na utashi wa kushughulikia changamoto lukuki zinazoikabili manispaa hiyo.
Alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni kushughulikia migogoro ya ardhi, kusimamia na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali katika kampuni na viwanda mbalimbali.
“Nimemudu uongozi wa Kamati ya Mipango Miji, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, nimeshughulikia kero mbalimbali na kutetea haki za wananchi na kupinga dhuluma dhidi yao, haya ni miongoni mwa mambo yanayonipa ujasiri wa kugombea umeya wa Ilemela,” alisema Matata.
Alitoa wito kwa wakazi wa Manispaa mpya ya Ilemela, kuimarisha ushirikiano na viongozi katika kushughulikia changamoto za maendeleo kwa manufaa ya Taifa.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment