Home » » MAASKOFU MWANZA WATOA TAMKO KUHUSU KATIBA

MAASKOFU MWANZA WATOA TAMKO KUHUSU KATIBA



Maaskofu, Wachungaji, Mapadri na Viongozi wa Makanisa Jijini Mwanza,
wakiwa katika picha ya pamoja kweny kanisa la Angalkana Mwanza, muda
mfupi kabla ya kutoa tamko kuhusiana na mchakato wa 
mabadiliko ya Katiba .
(Picha na Mashaka Baltazar wa Fullshangwe)

Na Mashaka Baltazar wa Fullshangwe-MWANZA

MAASKOFU,Wachungaji, Mapadri na Viongozi wa Makanisa
mbalimbali ya Kikristo Jijini Mwanza, wametoa angalizo kwa Serikali wakisema
vipo viashiria vya hatari vinavyoweza kuleta vurugu nchini.
 Kauli hiyo ilitolewa jana kwenye Kanisa la Anglikana hapa na
Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa ya Kikristo Jiji la Mwanza, Askofu Charles,  kwa niaba ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Jumuiya ya Maaskofu wa Makanisa ya
Kipentekosti Tanzania (CPTC )
 Alisema kuna viashiria vya hatari vinavyoweza kusababisha
vurugu nchini,hivyo ni  muhimu serikali
ikayaelewa kwa kutumia utawala, bunge na mahakama kwa maslahi ya Watanzania.
 Alisema viongozi wa makanisa wanasaidiana na serikali
kuongoza watu,lakini nchi ikienda vibaya Kanisa litalaumiwa kwa kuwa linaongoza
watu kiroho,wakati serikali ikiwatawala kwa kutumia sheria na katiba.
 “Mambo haya tunayozungumza tumeyafanyia utafiti na upembuzi
yakinifu, na tumeona tuzungumzie mambo muhimu yanayoikabili nchi yetu,baada ya
kukutana Sis Maaskofu, Wachungaji, Mapadri na Makanisa yote ya Kikristo,baada
ya kuona viashiria vya hatari katika taifa letu tunatoa tamko kwa mambo
yafuatayo,”alisema Sekelwa
  Alisema kwa kuwa serikali imeridhia kwamba mahakama ya Kadhi
iwe nje ya Katba na tayari Kadhi Mkuu na baadhi Makadhi wa mikoa wamekwisha
chaguliwa , hawaoni sababu tume ya marekebisho ya katiba kuendelea kuchukua
maoni ya suala ambalo limeshatolewa uamuzi na dini inayohusika.







 Kwamba kitendo kilichofanywa na serikali cha kuridhia na
kugharamia mafunzo ya watendaji wa Mahakama hiyo, ni ukiukwaji wa katiba ya
nchi iliyopo sasa.
 Kuhusu sheria za kidini za Zanzibar kwa mujibu wa tamko hilo
viongozi wa dini ya Kikiristo,walisema,kwa kuwa Jamhuri Muungano wa Tanzania
siyo ya kidini, hawaoni sababu wananchi wa Zanzibar  kulazimishwa kutii sheria za mfungo wa
Ramadhani kama Waziri Mkuu Mizengo Pinda alivyotoa majibu katika kikao cha
Bunge kinachoendelea.
 Majibu hayo ya Waziri Pinda yalitoa picha kana kwamba Zanzibar ni nchi inayoongozwa na mfumo wa sheria za kidini,
wakati Zanzibar
ni sehemu ya Jamhuri na serikali haina dini kwa mujibu wa katiba.

 Mgawanyo wa madaraka
 Viongozi hao walisema si sahihi kupokezana uongozi wa juu wa
nchi katika sehemu mbili za Bara na Visiwani , bali nafasi hiyo zingatiwe uwezo
wa Mtanzania wa kuongoza,maadili yake,uzoefu wake,wala kusiwe na ubaguzi wa
jinsia,hali, ukanda,ukabila na udini.
 Walisisitiza katika tamko hilo kutokuwepo kwa uwiano wa
udini katika uongozi wa juu wa nchi kwa vile serikali haina dini, kupokezaana
madaraka kwa misngi ya uwiano wa kidini kutaongeza chuki na migogoro isiyo na
tija kwa wananchi wa Tanzania.
 Walidai kupokezana madaraka kwa misingi ya udni usiwepo kwa
vile zipo dini nyingi sana
na kila moja na haki sawa, hakuna iliyo juu ya dini nyingine katika mfumo na
sera ya serikali
 Majengo ya Ibada kwenye ofisi za serikali
 Aidha tamko hilo linasema kwa
vile  serikali imeona vyema kuwa na majengo
ya ibada kwenye ofisi zake,basi fursa zilizosawa zitolewe kwa kila dini kuwa na
jengo lake kwenye ofisi hizo.
 Askofu Sekelwa alisema, kwa Rais na Wabunge ambao ni watunga
sera wanachaguliwa na wananchi ambao ni waumini wa dini mbalimbali , muhimu
kuyaelewa mambo hayo kwa kutumia utawala, bunge na mahakama kwa maslahi ya
Watanzania.
 Tamko hilo ambalo nakala yake tunayo limesainiwa na baadhi
ya Maaskofu, Wachungaji na  Mapadri wa
Jumuiya za makanisa ya TEC, CCT na CPTC ya Jiji la Mwanza, halikuwashirikisha waumini
wa dini za Kiislamu na Kihindu.
 Askofu Selekwa alisema sababu ya kutoshirikisha mdini za Kihindu na
kiilaslamu kunatokana na makanisa hayo kuamini  katika imani moja ya
dini ya Kikristo.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa