Mwandishi wetu, Mwanza
Serikali katika Wilaya ya Maswa imeamuru kusimamishwa kwa Mkandarasi wa Ujenzi wa Choo cha Wanafunzi katika shule ya msingi Sola baada ya kubainika kuwepo kwa udanganyifu katika fedha zilizotumika.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Maswa Luteni Abdalah Kihato kwa wandishi wa habari aliyo itoa leo Ofisini kwake
Mkuu wa Wilaya ameamua kutoa agizo hilo baada ya kupata maelezo kutoka kwa Kaimu Afisa Elimu wa Halimashauri ya Maswa, Martin Mahinda kuwa ujenzi wa choo hicho chenye Matundu 12 unatarajia kugharimu kiasi cha sh,15,000,0000 hadi kukamilika.
Luleni Kihato amebainisha zaidi kuwa gharama za ujenzi wa choo matundu 12 zinaonesha kuwa kuna mpango wa kufuja fedha za Serikali na watu walio pewa dhamana ya kusimamia miradi ya serikali wakishirikiana na wakandarasi wasio waminifu
Alipoulizwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Maswa ili atoe ufafanuzi juu ya tuhuma ya kuidhinisha zabuni ya Ujenzi wa choo matundu 12 kwa gharama ya Sh.15, 000,000.
Kwa upande Kaimu mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya Maswa Bwana Samweli Simbila amekiri kutolewa kwa Kandarasi hiyo na kimtaja mtu aliyepewa kuwa ni Kampuni ya Magembe ambaye Mmiliki wake ni Bwana Wiliamu Shilingi mkazi wa Malampaka Wilayani Maswa
Pamoja na mambo mengine Kaimu Mkurugenzi huyo amesema kuwa baada ya kufika eneo la ujenzi ametoa malekezo kwa Mhandisi wa Ujenzi kusimamisha kazi hiyo hadi atakapo elekeza vinginevyo
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment