Home » » WALIMU UKEREWE WARIDHIA MGOMO

WALIMU UKEREWE WARIDHIA MGOMO


na Jovither Kaijage, Ukerewe
ASILIMIA 92.5 ya walimu katika Wilaya ya Ukerewe, Mwanza wamepiga kura ya ndio ya kutaka ufanyike mgomo ikiwa ni hatua ya mwisho ya kuishinikiza serikali kuboresha maslahi yao.
Katibu wa Chama cha Walimu (CWT) wa wilaya hiyo, John Kafimbi, alisema hayo jana alipokuwa akizungumzia hatua zilizofikiwa kati ya serikali na chama hicho za kutatua mgogoro huo.
Alisema baada ya pande hizo mbili kushindwa kumaliza mvutano huo katika meza ya mazunguzo, sasa imefuata hatua ya walimu kupiga kura, ili kupata uhalali wa kwenda katika hatua ya mwisho ya mgomo.
Alisema walimu na wanachama wa CWT wapatao 1,810 wa wilaya hiyo wapo tayari kushiriki mgomo na kwamba hadi sasa ofisi yake imepokea kura 1,688 kati ya hizo za ndio ni 1,675 sawa na asilimia 92.5.
Aliyataja madai ya walimu kuwa ni nyongeza ya asilimia 100 ya mshahara, posho za kufundisha masomo ya sayansi asilimia 55 na somo la sanaa asilimia 50 wakati huo wanadai posho ya asilimia 30 ya kufanya kazi katika mazingira magumu.
Chanzo: Tanzania Daima


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa