Mwezeshaji wa mafunzo ya habari za biashara na uchumi Bw. Mnaku Mbani akitoa maelezo juu ya uandishi wa habari za Biashara na Uchumi, mafunzo yanayofanyika katika ukumbi wa Nyakahoja jijini Mwanza. |
Waandishi wa habari mkoa wa Mwanza wamepatiwa mafunzo ya uandishi wa habari za biashara na uchumi ili kuifanya jamii kupata uelewa zaidi kuhusu masuala mwelekeo wa taifa.
Akitoa elimu hiyo, muwezeshaji wa mafunzo hayo Bw. Mnaku Mbani amesema lengo la semina hiyo ni kuwanoa wanahabari nchini kuwa na uelewa katika masuala ya uchumi.
Mbani amesema hatua hiyo imekuja kutokana na waandishi wengi kutojikita katika uandishi huo wa habari za biashara na uchumi na hivyo eneo hilo kutotendewa haki licha ya kuwa muhimu.
Baadhi ya washiriki kutoka kushoto ni Chonya Libe Mathias, Albert G. Sengo, Levocatus Musese na Florah Magabe. |
Engo ya washiriki kushoto ni Florah Magabe, Anastazia Fredy na kwa chati aliyegeuza uso ni Maria wa Kwaneema Fm. |
Jumla ya waandishi 19 wamehudhuria mafunzo hayo yanayotaraji kumalizika siku ya alhamisi. |
Mafunzo hayo yaliyoanza siku ya jumatatu huku yakiratibiwa na Umoja wa chama cha waandishi wa habari Tanzania (UTPC) yamepangwa kufanyika kwa muda wa siku nne ambapo rasmi yatahitimishwa alhamisi ya tarehe 18july 2012 kwa majumuisho ya yote yaliyofanyika.
Chanzo:http://ujanatz.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment