Home » » Nyanza yajipanga upya

Nyanza yajipanga upya


na Sitta Tumma, Mwanza
MWENYEKITI wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Mwanza (Nyanza), Leonald Bogomola, amesema ushirika huo umejipanga kuhakikisha unapiga hatua kubwa kimaendeleo, ili kuinufaisha jamii wakiwemo wakulima wa zao la pamba.
Bugomola aliyasema hayo juzi jijini hapa wakati akizungumza na Tanzania Daima muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuiongoza Nyanza kwa mara ya pili mfululizo hivi karibuni.
Alisema kuwa Nyanza imedhamiria kuona inafikia malengo yake kwa kukuza zaidi uchumi wake na wateja wake kwa ujumla, na kwamba mikakati iliyopo ni kudhibiti kabisa matumizi mabaya ya fedha za ushirika huo na kuwashughulikia wabadhirifu wa mali za ushirika huo.
“Nyanza tumejipanga kisawasawa kupanua wigo wa kimaendeleo. Wananchi wanachotaka ni kuona wananufaika na ushirika huu...hatuna muda wa kupoteza katika kuhakikisha uchumi wa Wananyanza unakua,” alisema mwenyekiti.
Katika uchaguzi huo, mbali na Bugomola pia wajumbe wa mkutano mkuu wa ushirika huo waliwachagua wajumbe wanne wa bodi, wawakilishi wa ndani na nje ya bodi, huku Modesta Bulugu akichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa Nyanza.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa