Meli ikiwa inazama
Majina ya walio tambuliwa
Mnara wa kumbu kumbu
Makaburi
Hivi ndivyo ulikuwa uokoaji
Hili ni bango lilipo kwenye makaburi ya pamoja yaliyopo Igoma jiji Mwanza.Kutokana na miili ya walio wengi kuharibika na maji na hivyo kushindwa kutambuliwa na sababu zingine ilipelekea wapendwa wetu wapumzishwe kwenye makazi yao ya kudumu hapo.
********
Mei 21,1996 katika ziwa Victoria,Mwanza Tanzania meli ya Mv Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha yao.Meli ilizama kilomita 30 kukaribia kutua nanga kwenye bandari ya mwanza ikitokea Bukoba.
Meli ikuwa na uwezo wa kubeba idadi ya watu 430. Kwenye first and second class orodha ya abiria ilikuwa 443 na kwenye third class hakukuwepo rekodi yoyote .Takribani 1000 walifariki kwenye ajali hiyo.
Afrika ya kusini ilibidi kutoa msaada wa wanamaji wake waje kutusaidia kufanya uzamiaji wa kina kirefu kwani tulikuwa hatuna hivyo vifaa na utalaamu(sijui inagharimu kiasi gani kuvipata vifaa na utalaamu)
Meli ilikuwa na ubovu lakini iliruhusiwa kuendelea na kazi kama kawaida.(nani anajali au kuwajibishwa?)
Vifaa vya uokoaji mfano majaketi(life jacket) n.k na vitu kama hivyo vilikuwepo vya kutosha?( au hakuna uzembe wa viongozi..ni kazi ya Mungu kama walivyozoea kusema)
0 comments:
Post a Comment