Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2, 2018 tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam wakati akielezea maandalizi kabambe ya
Tamasha la pasaka linalotarajia kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa
CCM Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 tamasha
hilo litafanyika katika uwanja wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani
Simiyu.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
Mwimbaji Mahiri wa nyimbo za Kiroho (Injili) Rose Muhando
anatarajia kuizindua albamu yake ndani ya Tamasha la Pasaka
linalotarajiwa kufanyika kufanyika Aprili mosi katika uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza na baadae tamasha hilo April 2,2018 litafanyika
katika uwanja
wa Halmashauri ndani ya Bariadi mkoani Simiyu .
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama ambao ndiyo waandaaji wa
tamasha hilo, amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri na
wanatarajia kuanzia katika jiji La Mwanza ndani ya Uwanja wa CCM-Kiruma
Aprili 1, 2018 na kuelekea uwanja wa Halmashauri mjini Simiyu.
"Kwa kipindi kirefu Mwimbaji Rose Muhando amekuwa kimya kwa muda
mrefu ila kwasasa namtangaza Kinara Rose Muhando ndiyo atakayeongoza
jahazi la Tamasha la Pasaka kwa Mwaka 2018 hivyo wananchi mjitokeze kwa
Wingi," amesema Msama.
Aliongeza kuwa mbali na uzinduzi huo, tukio lingine kubwa
litakalofanyika ni kuombea nchi amani,hukua kauli mbiu itakuwa "Upendo
na Amani"
"Nipende kuwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika tamasha la
Pasaka ambalo litakuwa la namna yake na waje wajionee vipaji lukuki
kutoka ndani ya Tanzania na nje.
0 comments:
Post a Comment