Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia) akiuelezea Ugeni kutoka TADB kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba.. wanaomsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kulia), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati). Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Joseph Mutashubilwa (kushoto) na Bw. Dome Malosha (wapili kushoto).
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akihoji masuala mbalimbali kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba wakati alipouongoza ugeni kutoka TADB kutembelea Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza. Wanaomsikiliza ni Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Anuruphus Mpanju (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (wapili kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia).
Meneja Mradi wa Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju, Bw. Artem Ivanieiev (kushoto) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kulia) kuhusu Shamba la Kutotoleshea vifaranga vya samaki vya Kampuni ya Mpanju.
Sehemu ya vizimba vya kukuzia samaki vinavyomilikiwa na Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju.
Na mwandishi wetu, Mwanza.
Wadau
wa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (fish caging) mkoani
Mwanza wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB)
kuwasaidia katika kuendeleza tasnia iyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji
mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa samaki
mkoani humo.
Wito
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju,
Bw. Elpidius Mpanju Akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipotembelea
kujionea maendeleo ya tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba mkoani
Mwanza.
Bw.
Mpanju alisema kuwa ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za
mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika tasnia hiyo mpya ya
ufugaji wa samaki imekuwa inawapa changamoto katika uendelezaji wa
tasnia hiyo yenye faida lukuki kwa maendeleo ya kiuchumi nchini.
Bw.
. Mpanju aliongeza kuwa ukosefu wa mikopo ya uhakika imekuwa inarudisha
nyuma ukuaji wa tasnia hiyo mpya nchini kwa kuwa mahitaji mengi kwa
ajili ya kuhudumia ufugaji wa samaki inapatikana nje ya nchi hivyo
kuhitaji kiasi kikubwa cha mtaji.sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.
“Uduni
na ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo
mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa
biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo
tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.
Akijibu
changamoto hizo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo
ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa Serikali
iliamua kuanzisha Benki ya Kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu
ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta
ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika kilimo nchini.
0 comments:
Post a Comment