Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu
(kulia), akihutubia wakati akizindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani
Mwanza jana ambalo liko ndani ya
Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada
ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la
Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni. Kushoto ni Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu na katikati ni Mwenyekiti wa Bodi MSD,
Profesa Idrisa Mtulia.
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. Umy Mwalimu
(kushoto), akiwa na viongozi mbalimbali wa MSD wakati wa uzinduzi wa
duka hilo.
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
WAZIRI
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto. UmyMwalimu
amezindua rasmi duka la Dawa la MSD mkoani Mwanza ambalo liko ndani ya
Hospitali ya SekouToure, nakufanya maduka ya MSD yaliyofunguliwa baada
ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kufikia mawili baada ya lile la
Muhimbili lililofunguliwa mwaka jana mwishoni.
Katika
hotuba yake ya uzinduzi wa duka hilo, ameipongeza MSD kwa hatua hiyo
nzuri ya kufungua maduka ili kuwawezesha wananchi kupata dawa, na
kuitaka MSD kukamilisha ufunguzi wa maduka mengine mawili yaliyosalia
katika mikoa ya Arusha naMbeya, kwani hicho ni moja ya kipaumbele katika
uongozi waserikali ya awamu yaTano.
Waziri
huyo ameeleza kuwa Wizara yake imejiwekea malengo ya upatikanaji wa
dawa nchini kutoka asilimia 70 kwa sasa kufika hadi asilimia 95.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema maduka
mawili ya Arusha naMbeya yamemekamilika, na yanatarajia kufunguliwa hivi
karibuni, na kwamba kwa mikoa mingine wameshafanya mawasiliano na
kwamba tayari MSD imefanya mazungumzo na viongozi wa mikoa Ruvuma,
Rukwa, Singida, Dodoma, Geita, Kagera na Iringa kufungua maduka yao ya
dawa ambapo MSD itawauzia dawa.
“Tutakachofanya, sisi (MSD) utawapa utaalamu na kuwawezesha utaalamu wa uendeshaji maduka hayo” alieleza Bwanakunu.
0 comments:
Post a Comment