Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Lorietha Laurence- Maelezo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja Ndege nchini (TAA) Bw Suleiman Suleiman ametoa ufafanuzi
kuhusu hitilafu ya umeme iliyotokea katika uwanja wa ndege wa Mwanza
kuwa imetokana na marekebisho ya kangavuke (generator) ya dhalula katika
uwanja huo.
Bw. Suleiman ameeleza hayo leo
jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii
na kuongeza kuwa kila kiwanja cha ndege nchini kina generator ya
dhalula.
“Viwanja vyote vya ndege nchini
vina generator za dhalula, lakini kwa upande wa Mwanza hivi karibuni,
generator hiyo ilipata tatizo la kiufundi na taarifa ilitolewa kwa
makampuni yote ya usafirishaji wa abiria wanaotumia uwanja huo” alisema
Bw. Suleiman. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo,
mamlaka imeshafanya utaratibu wa kununua generator mpya itakayofungwa
katika uwanja wa ndege wa Mwanza wakati wowote kuanzia sasa kutatua
tatizo hilo.
Aidha Mkurugenzi huyo wa TAA
nchini ameeleza kuwa pamoja na tatizo la kukatika umeme katika uwanja wa
ndege wa Mwanza, hali ya usalama katika uwanja huo pamoja na viwanja
vingine nchini iko vizuri.
“Pamoja na tatizo hili,
nawahakikishia wasafiri wanaotumia viwanja vya ndege nchini na
watanzania kwa ujumla kuwa hali ya usalama katika viwanja vyetu
imethibitiwa,” amesema.Tanzania ilishika nafasi ya pili
mwaka 1999 ilipokaguliwa na shirika la usalama wa usafiri wa Anga
Duniani ambayo hufanya ukaguzi kwa wananchama kuhakikisha kuwa nchi
wanachama wanafikia vigezo. Shirika hilo linatarajia kufanya ukaguzi
mwezi Septemba mwaka huu.
Hivi karibuni abiria wa kwenda
Mwanza kupitia kampuni ya usafirishaji ya Fastjet walihairishiwa safari
zao kutokana na hitilafu ya umeme katika viwanja vya ndege vya Mwanza
ambao ulikuwa ukifanyiwa matengenezo tangu ijumaa iliyopita.
0 comments:
Post a Comment