Watu tisa waliokuwa wakisafiri na gari dogo aina ya noah namba T812 BJU, wamefariki dunia papo hapo baada ya gari hilo kuacha njia na kupinduka jana jioni.
Ajali hiyo imetokea saa 11 jioni katika kijiji cha Mwamanga wilayani Misungwi mkoa wa Mwanza kwenye barabara kuu ya kutoka Shinyanga kuelekea Mwanza, wakati gari hilo kumshinda dereva wake ambaye ni koplo mstaafu wa jeshi, Moris Lukenza, mkazi wa Geita.
Kamanda Mkumbo amewataja waliofariki papo hapo katika ajali hiyo ni
pamoja na dereva, Moris Lukenza, Malongo Magongo, Shija Somanga, Yun Somanga, Thobias Simon, Michael Simon, Amos Lukenza, Shaban Deus na Samwel Malongo wote wakazi wa mkoani Geita.
pamoja na dereva, Moris Lukenza, Malongo Magongo, Shija Somanga, Yun Somanga, Thobias Simon, Michael Simon, Amos Lukenza, Shaban Deus na Samwel Malongo wote wakazi wa mkoani Geita.
Aidha, amesema katika ajali hiyo kulikuwa na majeruhi sita ambao hali zao zimeelezwa ni mbaya na kuwahishwa hospitali ya rufaa bugando jijini Mwanza.
Kamnada Mkumbo ametoa wito kwa madereva mkoani humo, kuzingatia sheria za usalama barabarani kwa lengo la kuepukana na ajali zisizo za lazima.
0 comments:
Post a Comment