Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MARA baada ya Cha cha mapinduzi CCM kuzinduliwa kampeni zake za uchaguzi kitaifa ndani ya jiji la Dar es salaam viwanja vya Jangwani, mbio za kampeni sasa zinaendelea kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini ambapo mkoa wa Mwanza unategemea kufanya uzinduzi wake kesho (jumatano) ya tarehe 26 August 2015 na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Mjumbe wa NEC Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji ambaye ni mbunge wa Mtera.
Kwa mujibu wa Katibu uenezi wa CCM Mkoa wa Mwanza Simon Mangelepa amesema kuwa uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya Mbugani wilayani Nyamagana kuanzia saa sita mchana hadi saa 12 jioni ambapo maandalizi yote yamekwisha kamilika.
Ameongeza kuwa Mhe. Lusinde ataambatana na mwenyeji wake katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza pamoja na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho kuwatambulisha madiwani wateule 19 wa wilaya ya Nyamagana na 18 kwa wilaya ya Ilemela
Majimbo mengine yaliyoalikwa kwenye uzinduzi huo ni pamoja na Magu, Sengerema, Ukerewe, BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
KWA HISANI YA GSENGO BLOG