Ofisa
wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza 7171
Josephine (kushoto), akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva Alex John
wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani humo
ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send”
inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi
wakati wakiwa wanaendesha kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Dereva
wa kampuni ya mabasi ya Mohamed Trans, Soud Nassoro (katikati) akitumia
kifaa maalum cha kupima kilevi huku askari wa kikosi cha usalama
barabara jijini Mwanza, F4278 PC Luge na Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda
ya Ziwa, Domicien Mkama akishuhudia wakati wa operesheni ya usalama
barabarani iliyofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo
ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send”
inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi
wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo.Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom
Tanzania.
Dereva
Lucas Kibogi akipuliza kifaa maalum cha kupima kilevi mwilini kama ana
kilevi mwilini wakati wa zoezi maalum la usalama barabarani
lililofanyika katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni
mwendelezo wa kampeni ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa
vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi i wakiwa wanatumia vyombo
hivyo. Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.
Ofisa
wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza Koplo
Jeremia akimpima kilevi kwa kutumia kifaa maalum dereva Nyange Migoko
(katikati) wakati wa zoezi maalum la usalama barabarani lililofanyika
katika kituo cha mabasi Nyegezi Mkoani humo ikiwa ni mwendelezo wa
kampeni ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto
kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanatumia vyombo hivyo.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment