HALMASHAURI ya Jiji la Mwanza wametakiwa kuangalia upya utaratibu wa utoaji wa zabuni za usafi kwa kuwapatia watu wanaoishi katika maeneo husika ili waweze kusimamia suala hilo, kwani ndio wanaoguswa.
Agizo hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo baada ya kutembelea kwenye stendi ya Nyegezi kukagua maagizo aliyoyatoa ya uwekwaji wa taa na kusafisha vyoo pamoja na dampo kama yametekelezwa ambapo alielezwa na Mhandisi kuwa hadi juzi jioni taa za stendi zingekuwa zimewaka.
“Hawa ndio waathirika wa uchafu katika maeneo haya kama mikataba ya kufanya usafi wangepewa wananchi wa maeneo hayo, haya tunayoyaona yasingekuwepo, uchafu huu upo kwa sababu mawakala waliopewa kazi hawaishi huku na hawaoni umuhimu wa kusafisha kila wakati,†alisema mkuu wa mkoa wakati akitoa maagizo kwa watendaji wa jiji akiwemo Kaimu Mkurugenzi, Mhandisi na Ofisa Afya.
Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment