UBOVU wa miundombinu na wataalam katika vyuo vya Utalii nchini,
unachangia kuikosesha serikali mapato kutokana na wanafunzi kutoka
mataifa mengine kushindwa kuja kusoma wakihofia ubora wa mafunzo
unaotolewa.
Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkuu wa Chuo cha
Taaluma ya Wanayama pori mkoani Mwanza, Lowaeli Damalu wakati wa
mahafali ya chuo hicho jijini hapa.
Alisema miundombinu mibovu katika chuo hicho umesababisha muhula wa
mafunzo mwaka 2014/15 wanafunzi kutoka Sudan na Msumbiji kushindwa
kuwasili kutokana na kuwepo ubovu wa miundombinu.
Alisema wananchi wanafahamu sheria za wanayama pori na utuzaji wa
mazingira lakini wanakiuka sheria hizo kitendo kinachoongeza uharibifu
wa misitu na uwindaji haramu.
Chanzo;Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment