Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba, amesema kamwe hawezi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwa anaamini katika itikadi za chama hicho na kwenye sera zake.
Aidha, amesema hataki kulumbana na watu wanaomkosoa na kumtaka atoke CCM kwa kuwa chama hakijamwandikia barua au kumpatia malalamiko rasmi.
Akizungumza na NIPASHE jana, Jaji Warioba ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema amekuwa mwanachama wa CCM kwa takribani miaka 53 na kwamba anaamini sera na itikadi za chama hicho.
“Na siwezi kutoka nikaenda mahali pengine kwa sababu niende kufanya nini kama sina imani na itikadi na sera za huko na wala siyo mara ya kwanza kutoa mawazo ambayo yanahitalifiana na baadhi ya viongozi,” alisema.
Alisema uhai wa chama hicho ni mapambano ya hoja miongoni mwa wanachama wake.
“Wakileta officcially (rasmi), kuna taratibu zake lakini naamini hiyo haipo, kwa hiyo msifuate watu wanavyoropoka.”
Alisema alipokuwa Mwenyekiti wa Tume hakuapa kuitumikia CCM, Chadema au CUF na kwamba alipewa kazi ya nchi na alichofanya ni kuratibu na kukusanya maoni ya wananchi.“Na Katiba hii itakuwa ya wananchi haitakuwa ya kikundi.”
Alisema Katiba ya nchi haiwezi kuwa ya makundi na kwamba nia ni kujenga Tanzania moja.

CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment