Tone

Tone
Home » » CHADEMA MWANZA YAJIPANGA KUIKABILI CCM

CHADEMA MWANZA YAJIPANGA KUIKABILI CCM

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Mwanza kimeandaa mbinu mbaya za kukiangamiza Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Kiongozi wa operesheni Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, alisema kuwa, hawatasita kuwaeleza wananchi vitendo wanavyovifanya baadhi ya wabunge wa CCM.
Alisema CCM imekuwa ikishindwa kusikiliza na kutambua matatizo yanayolikabili taifa, badala yake wamekuwa wakitumia nyadhifa zao vibaya kuihujumu nchi, kitendo kinachosababisha kuendelea kuwa masikini.
Njugu, alisema baadhi ya wabunge wanaotokana na CCM, wamekuwa wakishindwa kujadili mawazo ya wananchi kama yalivyokusanywa wakati wa mchakao wa kujadili rasimu ya katiba na kuweka kile watanzania walichokusudia kukipata.
“Tutawatumia walimu, wanafunzi na watumishi wa sekta ya umma kuhakisha watanzania wanapata katiba iliyo bora, hatuwezi kunyanyaswa na sisi tunaangalia, kuna baadhi ya vigogo wa CCM wanaona ile rasimu iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba inawabana ndo maana wanadiriki kupitisha mambo ambayo hayakuwemo,” alisema.
C;Tanzania Daimahanzo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa