Tone

Tone
Home » » 17 WAJERUHIWA KWA RADI MWANZA

17 WAJERUHIWA KWA RADI MWANZA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
17 wajeruhiwa kwa radi Mwanza
WANAFUNZI 17 wa Shule ya Sekondari ya Kabuholo wilayani Ilemela jijini Mwanza, wamejeruhiwa na radi.

Tukio hilo limetokea jana asubuhi ambapo radi iliwapiga wanafunzi 15 wa kidato cha nne, mmoja wa kidato cha tatu na mwingine kidato cha kwanza.
Akizungumzia tukio hilo, Mwalimu wa mazingira wa shule hiyo, Humphrey Massawe, alisema tukio hilo lilitokea wanafunzi hao wakiwa darasani ambapo mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali iilikuwa ikinyesha.
“Tulikuwa ofisini wakati mvua ikiendelea kunyesha walifika baadhi ya wanafunzi wakasema wenzao wa kidato cha nne wamepigwa na radi…nilipokwenda nikawakuta baadhi yao wakiwa wamepoteza fahamu huku Joyce Juma (19), akiwa amelala chini na ameng’ata ulimi na shati lake likiwa limeungua mgongoni,” alisema Massawe.
Muuguzi wa zamu katika katika hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure, Aquilina Shai, alisema waliwapokea wanafunzi 17 kutoka sekondari hiyo.
Aliwataja wanafunzi hao ni Jofrey Dioniz (19), Joyce Juma (19), Flora Magesa (18), Lucy Jonas, John Bwire (17), Yohana Zabron, Mohamed Edwin, Frank Cuthbert na Asimwe Joseph.
Wengine ni Aisha Juma, Lucy David, Hawa Musa, Faraja Richad, Anita Robert, Martha Zakaria na Neema Deus.
“Kati yao 14 miwongoni mwao waliruhusiwa baada ya kutibiwa huku watatu Joyce, Neema na Dioniz wakiwa wamelazwa kutokana na hali zao kuwa mbaya,” alisema Shai.
Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola, alisema bado hajapata taarifa kuhusiana na tukio hilo.
Chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa