Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MABINGWA wa Wilaya za
Nyamagana, timu ya Alliance School Sports Academy (ASSA) na Mwanza City
ya Ilemela, zimetoa onyo kwa timu zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa Mkoa wa
Mwanza.
Timu hizo ziliibuka na
ushindi mnono dhidi ya wapinzani wao, ambapo Alliance iliichabanga
Nyasaka FC kwa mabao 4-1 jana kwenye Uwanja wa Nyamagana.
Mwanza City ya kundi A,
nayo juzi kwenye uwanja huo iliibugiza Misungwi Winner kwa mabao 7-0,
huku mchezaji John K. John akipiga 'hat trick', mengine yakifungwa na
Ali Fadhil, Ismail Moba, Gwakisa Richard, Abdallah Abubakar na Dustun
Datty.
Katika mchezo wa jana,
Alliance iliyopo kundi B, ilijipatia bao la kuongoza dakika ya 23,
lililofungwa na mshambuliaji Abubakar Hamis na kudumu hadi mapumziko.
Iliwachukua Alliance
dakika saba tangu kuanza kwa kipindi cha pili kuandika bao la pili
kupitia kwa mshambuliaji wake hatari Athanas Mdamula, kabla ya Lameck
Philipo kufunga la tatu dakika ya 60.
Dakika moja baadaye
Mdamula tena aliwanyanyua mashabiki wa Alliance vitini baada ya
kupachika bao la nne ambapo Martin Kiggi alifunga kitabu cha mabao kwa
kufunga bao la tano dakika ya 88.
Bao la kufutia machozi la Nyasaka lilipatikana dakika ya 70 likipachikwa wavuni na Yahaya Shaaban.
Aidha juzi Stand
Express ya Misungwi ya kundi B ilifanya kweli kwa kuichapa Scud ya Magu
kwa mabao 4-1, katika mfululizo wa michuano hiyo.
Wafungaji wa mabao ya
Stand Express,walikuwa ni Dastubn Datty (2),Mhalu Masunga na Deusdedit
Okoya kabla ya Ribo Katu, kuifungia Scud bao la kufutia machozi.
Mchezo mwingine wa
kundi A uliokuwa uzikutanishe timu ya Usalama ya Magu dhidi ya New Stand
ya Ukerewe, haukufanyika baada ya Usalama kushindwa kutokea uwanjani.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa MZFA,Nassib Mabrouk,wanasubiri taarifa ya mwamuzi kabla ya kutoa uamuzi wa mchezo huo
Chanzo:Majira
0 comments:
Post a Comment