Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani, alipotembelea ujenzi wa kituo hicho jana, alisema kuwa Waziri mkuu ameahidi kutoa fedha hizo baada ya kuguswa na umuhimu wa kuwepo kwa kituo hicho. Alisema kituo hicho kitapunguza hofu miongoni mwa watoto wenye ulemavu kutoka mikoa ya Kanda ya ziwa. "Kabla ya kuja kutembelea ujenzi wa kituo hiki nimezungumza na waziri mkuu, Mizengo
Pinda...baada ya kumueleza kwa kina juu ya malengo ya kituo hiki ameguswa sana, na hivyo ameahidi kuchangia shilingi milioni tano," alisema Dk. Kamani.
Dk Kamani alisema, ujenzi huo umeshaanza na unatarajiwa kukamilika kabla ya mwishoni mwa mwaka kesho kwa gharama ya zaidi ya Sh. bilioni 1.5.
Alisema kituo hicho kitakuwa na uwezo kwa kuhifadhi watoto 100 kwa wakati mmoja watakaopewa huduma ya masomo bure.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment