Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
VIONGOZI wa serikali wametakiwa kutokuwa na kigugumizi cha
kuitaja Tanzania kuwa ni kinara katika usafirishaji wa dawa za
kulevya katika nchi zilizopo ukanda wa Jangwa la Sahara na
Afrika Mashariki, ili kuonyesha uhalisia wa tatizo na kulitafutia
ufumbuzi.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kupiga Vita Dawa za
Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko, alitoa kauli
hiyo mjini hapa alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari
kutokana na kauli ya Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (Tamisemi), Kassimu Majaliwa, juu ya ongezeko la
usafirishaji na matumizi ya dawa za kulevya nchini.
Alisema kama serikali na wadau wengine ikiwemo na taasisi ya
OJADACT kweli wana nia ya kupambana na janga hili, ni wazi
tukubali kujinyoshea kidole.
Soko alisema ripoti mbalimbali kama ya Umoja wa Mataifa
kupitia dawati lake la kupambana na mihadarati (UNODC) ya mwaka
2013, imetaja Tanzania kuongoza kwa kusafirisha dawa za kulevya
zikiwemo heroine na cocaine katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Alisema sababu kubwa ya tatizo hilo ni Tanzania kuwa na sheria
dhaifu ambazo kimsingi zimeshindwa kupambana na biashara hiyo
kama vile kutoa adhabu ndogo kwa watuhumiwa.
“Sababu nyingine ya kushamiri kwa biashara hiyo ni kukua kwa soko
la ndani la mahitaji ya dawa za kulevya, pamoja na mipaka ya
Tanzania kutokuwa na ulinzi wa kutosha katika vituo vya kuingilia
wageni kama bandari na viwanja vya ndege,” alisema.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment