Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umeiomba Serikali ya Mkoa wa
Mwanza kuupatia eneo la kujenga kitega uchumi chake ili kusogeza
huduma karibu na wananchi.
Ombi hilo lilitolewa jana jijini hapa na mjumbe wa NHIF, Dk. Raphael Chegeni, wakati wa mkutano wa wadau wa mfuko huo.
Alisema upo ugumu wa kuwafikia wananchi kwa kukosekana eneo linalofaa
kujenga ofisi mkoani hapa na maeneo mengine ya Kanda ya Ziwa, hivyo
kusababisha uhaba wa huduma bora kwa wanachama.
Alisema hadi sasa mfuko huo umepata maeneo mikoa ya Dodoma na Tabora
wanakotarajia kujenga vitega uchumi, na kuongeza kwamba jitihada za
kuboresha utendaji wa mfuko zinaelekezwa katika kupata hospitali na
vituo vya afya.
“Tangu tuanze kukopesha hospitali hapa nchini, walengwa ambao ni
sekta ya afya, wameshindwa kutumia fursa hiyo ili kupunguza matatizo
yao… hospitali iliyokopeshwa fedha nyingi kuliko zote ni Muhimbili
ambayo imechukua zaidi ya sh bilioni 17 na Bugando sh milioni tano japo
sio kiwango cha kuridhisha,” alisema Dk. Chegeni.
Chanzo;Tanznia Daima
0 comments:
Post a Comment