Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Matatizo yanayolikabili Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na
kususuasua kwa ukarabati wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza, ni miongoni mwa
mambo yaliyotishia kukwamisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya
Uchukuzi, bungeni juzi.
Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM),
alitoa shilingi akitaka maelezo ya kina juu ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege
wa Mwanza.
Chenge aliungwa mkono na mbunge wa Sumve, Richard
Ndassa (CCM), aliyesema hata mshauri mwelekezi anaidai wizara mamilioni
ya fedha, huku mbunge wa Busanda, Lorencia Bukwimba (CCM) na mbunge wa
Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema) wakiungana nao kuzuia mshahara wa
waziri.
Sakata hilo lilimlazimisha Waziri wa Fedha, Saada
Mkuya, kulieleza Bunge kuwa Hazina itatoa Sh6.4 bilioni kabla ya mwaka
huu wa fedha kwisha ili kupunguza madeni ya wakandarasi wa uwanja huo.
“Tutakutana na Kamati ya Bajeti kuangalia
uwezekano wa kuongeza fedha kwa ajili ya uwanja huo,” alisema Mkuya na
kumshawishi Chenge kurudisha shilingi.
Sakata la ATCL
Wenje naye aling’ang’ania shilingi ya mshahara wa
waziri akitaka kufahamu waliohusika na ubadhirifu wa Shirika la ATCL na
wamechukuliwa hatua gani na lini deni litalipwa.
Alisema viwanja vingi vimejengwa nchini, lakini Serikali inasema haiwezi kununua ndege kwa sababu zitakamatwa na wadeni.
Amkijibu Dk Mwakyembe, alisema suala hilo lipo
Takukuru na waliohusika wameshafikishwa mahakamani. Alisema wameandika
waraka kwenda Baraza la Mawaziri ili Serikali ichukuedeni hilo ili ATCL
ianze kufanya kazi.
Hata hivyo, Wenje alisema katika bajeti nzima ya Wizara ya Uchukuzi hakuna sehemu ambayo inaonyesha madeni hayo yatalipwa lini.
Aliwaomba wabunge wenzake wajadili kwa pamoja ili Serikali itoe muda ni lini watalipa deni ili nchi ipate ndege.
Kwa upande wake Freemon Mbowe, (Chadema), alisema yeye ni mmoja wa watu wanaoidai ATCL Dola 200,000 za Marekani.
Chanzo;Mwananch
Alisema ATCL inamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na kwamba
haiwezi kujivua madeni yake, hivyo kuitaka itoe kauli ya lini watalipa
madeni hayo.
Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema (Chadema),
alisema wabunge wanawaonea mawaziri wa Uchukuzi kwa kuwataka kununua
ndege wakati Serikali imeshindwa kununua madawati shuleni.
Naye Peter Serukamba aliitaka suala hilo limalizwe haraka ili shirika hilo liweze kununua ndege.
Chanzo;Mwananch
0 comments:
Post a Comment