Home » » UKOSEFU WA SARAFU MOJA NI TATIZO KIUCHUMI

UKOSEFU WA SARAFU MOJA NI TATIZO KIUCHUMI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

IMEELEZWA kuwa kutokuwepo kwa matumizi ya sarafu moja katika soko la pamoja la Afrika Mashariki kumeleta athari kubwa zitokanazo na matumizi makubwa ya fedha za kigeni katika nchi wanachama wa jumuia hizo.
Hayo yalielezwa jana na mwezeshaji kutoka makao makuu ya Benki ya CRDB, Ngeleja Mcharo katika semina ya wanahisa wa benki hiyo iliyofanyika mjini hapa yenye lengo la kukuza uelewa wa soko la mitaji.
Mcharo alisema kuwa matumizi ya fedha za kigeni katika soko la mitaji la Afrika Mashariki yameleta changamoto hususan kwa wafanyabiashara katika nchi hizo.
Akizungumza kwa upande wa wafanyabiashara wa Tanzania, Mcharo alisema wanashindwa kuhimili ushindani wa soko la pamoja kutokana na kutokuwa na mitaji mikubwa, hali itasababisha wafanyabishara wa nje kushikilia soko hapa nchini.
Kwa upande wao washiriki wa semina hiyo walisema kuwa semina za elimu ya hisa ziwepo mara kwa mara ili kuwajengea uwezo zaidi wanahisa juu ya masuala ya kukuza mitaji .
Awali akifungua semina hiyo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Kahama Luther Mneney aliwataka wanahisa kuifanya benki ya CRDB kama mali yao na kwamba wazidi kununua hisa kwa faida zao na bodi ndiyo msimamizi.
Mneney alisema kwa sasa vijana wengi hawataki kujua mambo ya kibenki kama ya kukuza mitaji au mambo ya hisa, hali ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa kutokuwa na uelewa kuhusu mambo ya kibenki.
Chanzo:Habari Leo

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa