Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MEYA wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula, ameupongeza uongozi wa
Kampuni ya Tanzania ya Chemicotex, inayotengeneza mafuta ya nywele na
vipodozi vinavyotokana na tunda la parachichi, kwa jitihada zake za
kupanua ajira kwa vijana nchini.
Meya Mabula alitoa pongezi hizo mjini hapa juzi kwenye uzinduzi wa
mafuta na vipodozi aina ya Tressa, ambayo yameelezwa kutibu magonjwa ya
ngozi, mba na kuongeza vitamini mwilini.
“Nawapongezeni kwa kuanza uzalishaji wa mafuta ya nywele na
vipodozi vinavyotokana na tunda la parachichi. Hakika vijana wengi
watanufaika navyo kwa kuanzisha biashara za saluni,” alisema.
Meneja Biashara na Masoko wa kampuni hiyo, Manoj Kumarm, alisema
vipodozi vinavyoingizwa nchini kutoka nje ya nchi vimekuwa vikileta
madhara makubwa kwa Watanzania, kutokana na kutengenezwa kwa kemikali
kali, na aliwaomba Watanzania kutumia Tressa inayotokana na matunda ya
parachichi.
Alisema mbali ya Tressa kutunza nywele na kung’arisha mwili, pia
inaongeza vitamini mwilini, na alitaja bidhaa nyingine wanazozalisha
kuwa ni dawa za meno aina ya Whitedent.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment