Home » » JOYCE NYEMBA AKWAA TUZO YA MWANAMKE JASIRI 2014

JOYCE NYEMBA AKWAA TUZO YA MWANAMKE JASIRI 2014

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Balozi Mdogo wa Marekani nchini Tanzania, Virginia Blaser (kushoto), akimkabidhi Tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania ya mwaka 2014, Joyce Nyembe kwenye hafla iluyofanyika nyumbani kwa balozi huyo jijini Dar es Salaam jana.PICHA: KWA HISANI YA UBALOZI WA MAREKANI
Joyce  Nyembe (56), mkazi wa mkoani Mwanza, ametunukiwa Tuzo ya Mwanamke Jasiri wa Kitanzania ya mwaka 2014.
Nyembe alitunikiwa Tuzo hiyo jijini Dar es Salaam jana na Balozi Mdogo wa Marekani nchini, Virginia Blaser, kutokana na harakati zake za kupigania afya ya jamii na kupinga ukatili wa kijinsia.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Balozi Blaser alisema kuwa Nyembe anakuwa wa nane kutunukiwa tuzo hiyo toka ilipoanzishwa 2008.

Alimpongeza kwa kazi yake nzuri ya kutetea haki za wanawake pamoja na watoto katika jamii ya Mwanza.

Kwa upande wake, Nyembe alisema kuwa Tuzo hiyo imemtia nguvu na kumpa hamasa kubwa na nguvu ya kufanya kazi kwa bidii ili kuwakomboa na kuwatetea wanawake na watoto ambao bado wananyanyaswa na kuteswa ikiwa ni pamoja na kunyanyapaliwa katika jamii.

“Kwa hakika hii ni bahati kubwa sana kwangu na ya kipekee, kwani mimi ni mama wa kawaida na wa ngazi ya chini kabisa kiutendaji, lakini leo hii nimetambuliwa na Ubalozi wa Marekani nchini," alisema.
 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa