BAADHI
ya wakazi wa wilaya ya Ukerewe, Mwanza
wamelizishwa na utendaji wa mfuko wa jimbo hilo kipindi
hiki tofauti na hapo nyuma ambapo akuna kumbukumbu
miradi iliyotekelezwa na mfuko huo.
Wakazi
hao walieleza hayo jana katika mkutano wa adhala
ulioitishwa na mtandao wa asasi za kirai wa
wilaya hiyo [Ungonet] na kuwasilisha ripoti yake
ya uchunguzi ya kupima ufanisi wa mfuko huo katika
kipindi cha mwaka 2010/012.
Katibu
wa Ungonet Leocadia Vedastus aliwaeleza
wananchi waliouzulia mkutano huo katika kijiji cha Bukongo
kuwa mbali ya mafanikio yaliyopo pia
wamebaini mapungufu kadhaa ikiwemo baadhi ya miradi kutekelezwa
chini ya kiwango .
Akisisitiza
ukubwa wa tatizo hilo mbali ya kutaka
kamati ya mfuko huo ipewa nguvu ya kisheria ya
kusimamia shughuri zake alikwenda mbali zaidi na kutaka
mwandisi wa ujenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo
achunguzwe ili kubaini kama ana sifa zinazostaili kuwa katika
nafasi hiyo.
Akichangia
maoni yake Padri Charles Masaga wa kanisa katoriki
parokia ya Nansio alisema mbali ya
mapungufu yaliyopo lakini uongozi wa sasa wa mfuko
wa jimbo ni vyema ukapongezwa tofauti na ilivyokuwa hapo
nyuma.
Alisema
katika kipindi hiki miradi iliyotekelezwa na fedha ya mfuko huo
ikiwemo kituo kipya cha magari , masoko na miradi mingine
vinaonekana hivyo kuthibitisha matumizi ya fedha
ya mfuko huo katika miradi ya kijamii.
Naye
Majuto Mkama mbali ya kutojua shughuri za mfuko
huo pia alitaka taarifa ya kiasi kinacholetwa kila mwaka
na matumizi ya fedha za mfuko wa jimbo tangu
uanzishwe hapo mwaka 2005.
Alisema
shughuri hiyo inayofanyika sasa hapo nyuma aikufanyika hivyo
imekuwa sababu kubwa ya wananchi wengi mbali ya
kutofaamu shughuri za mfuko huo pia akuna miradi iliyotekelezwa kwa
fedha ya mfuko huo kati ya mwaka 2005/09.
Katibu
wa mbunge wa jimbo hilo Mathias Chilebelo
alisema aelewi chochote juu ya fedha za mfuko wa jimbo
zilizoletwa kipindi hicho cha 2005/09 na kuongeza kuwa kati ya
mwaka 2010 hadi sasa wamepokea na kutumia sh. Mil 115.3.
Alisema
fedha hizo zimetumika kutekeleza miradi 17 ya
aina mbali mbali ya kijamii katika sekta za kiuchumi, elimu, afya ,
uchukuzi na mazingira na kuongeza kuwa wakati anapokea
ofisi aikuwa na kumbukumbu ya shughuri za aina yoyote zilizofanyika
hapo nyuma.
Alisema
zipo sifa na vigezo vinavyotumika kutoa fedha hizo kwa
kila jimbo ikiwemo kigezo cha cha idadi ya watu na kuongeza
kuwa jimbo hilo linatakiwa kupokea sh. Mil. 84 kila mwaka
lakini fedha wanayopokea imekuwa chini hapo na kusababisha
miradi iliyolengwa kutotekelezwa kwa wakati.
Ikumbukwe
hapo mwaka 2010 aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
kwa tiketi ya ccm Getruda Mongera alishindwa na
Salvatory Machemli wa Chadema katika uchuguzi mkuu
uliopita.
0 comments:
Post a Comment