Home » » PPF yataka wafanyakazi wawe huru kuchagua mfuko

PPF yataka wafanyakazi wawe huru kuchagua mfuko

MFUKO wa Pensheni wa PPF, umewataka waajiri kote nchini, kuwapatia nafasi wafanyakazi wao kuchagua aina ya mfuko wa hifadhi wa jamii, wanaouona una manufaa kwao badala ya kuwalazimisha. Ushauri huo, umetolewa na Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Mfuko wa Hifadhi wa PPF, Meshack Bandawe wakati akizungumza na Maofisa Rasilimali Watu (HR) wa makampuni ya migodi ya dhahabu na madini.
Alisema wafanyakazi wanaelewafika, ni mfuko upi wa hifadhi ya jamii ambao una manufaa kwao na kwa mujibu wa muongozo uliotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), ni marufuku kwa waajiri kuwachagulia wafanyakazi wao mifuko ya hifadhi ya jamii ya kujiunga nayo.

Alisema PPF, imekuwa ukiongoza kwa wafanyakazi pamoja na taasisi binafsi kujiunga kila mwaka, kutokana na kutoa mafao mengi zaidi kwa wanachama wake tofauti na mifuko mingine ya hifadhi ya jamii.

“Mafanikio ambayo imekuwa ikiyapata PPF na kuungwa mkono na wanachama wake ni namna ambavyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanachama wake wananufaika na mfuko huo na kuwataka wananchi zaidi kujiunga na mfuko wa PPF, kwa ajili ya kupata manufaa kutokana na mafao na huduma zinazotolewa na mfuko huo,” alisema Bandawe.

Katika hatua nyingine mfuko wa PPF, umeyapongeza makampuni ya migodi yaliyopo katika kanda ya ziwa kutokana na kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati na kuyataka makampuni mengine kuiga mfano huo.

chanzo: MTANZANIA

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa