Home » » VIJANA CHADEMA CHUO CHA SAUT WAJADILI HALI YA KISIASA MWANZA NA KIFO CHA RPC LIBEARTUS BALLOW.

VIJANA CHADEMA CHUO CHA SAUT WAJADILI HALI YA KISIASA MWANZA NA KIFO CHA RPC LIBEARTUS BALLOW.


Na Derick Milton Mwanza.
Kufatia kutokea mauji ya kinyama kwa mkuu wa polisi mkoani mwanza Liberat Barolw usiku wa kuamkia jana maeneo ya kitangili ilemela jijini mwanza jumuiya ya vijana wa chama cha Demokrasia na Maendeleo[CHADEMA]  kutoka chuo kikuu sauti jijini mwanza  wamejadili hali ya kisiasa na usalama wa raia katika jiji  la mwanza na kusema kuwa ni lazima serikali kuimarisha ulinzi wa nguvu  ili kuweza kulinda raia wake.

Wamesema kuwa kutokana na tukio hilo lililoshutua watu wengi hasa wa mkoa wa mwanza limeonyesha ya kuwa hali ya usalama katika jiji la mwanza bado ni dhaifu sana na kunaitajika nguvu za ziada kutoka kwa vijana kuweza kulizungumzia hili ili kuweza kuwa na ulinzi imara.

Wamesema kuwa kutishiwa kwa Afisa uamiaji mkoa wa mwanza hivi karibuni kabla ya tukio la mauaji ya kamanda Barolw  matukio hayo yote yameonyesha dhaili  kuwepo kwa udhaifu katika sekta ya ulinzi ukilinganisha na wingi wa watu ndani  jiji na  kuwepo kwa mwingiliano wa watu wengi kutoka katika sehemu nyingi kanda ya ziwa na nchi za jirani.

Kwa pande wake mwenyekiti wa vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo [CHADEMA] kutoka katika chou hicho  Petrobass Paschal [Mwanasheria] amesema kuwa ni vyema kama vijana kuchukua uamuzi wa kuweza kupambana na matukio  kama haya.

Amesema kuwa kama hili limetokea kwa  kiongozi amabye anatakiwa  kuhakikisha wananchi wanakuwa katika hali ya usalama kwa mda wote pamoja na mali zao kauwawa, vipi usalama wa raia pamoja na mali zao kuwa salama kwa mda wote?

Aidha vijana hao wamezungumzia hali ya kisiasa katika chama chao[CHADEMA] na mkoa kwa ujumla mara baada ya chama chao kushindwa kuliongoza jiji la mwanza  kwa mara nyingine [MEYA NA NAIBU MEYA] pamoja kutimliwa uanachama kwa madiwani wawili wa chadema jijini mwanza.

Wamesema kuwa kama vijana watatoa tamko kuhusiana na matukio hayo ya kisiasa ndani ya chama chao mara baada ya kutafuta ukweli kutoka pande mbili[walalamikaji na walalamikiwa] ili kuweza kujua chanzo cha tatizo ni wapi na kuweza kutoa ushauli ndani ya chama kwa ngazi ya juu.

Amewataka wanafunzi hao kuweza kutumia elimu  pamoja na ujuzi wanaopata chuoni na ndani ya masomo yao kweza kelimisha jamii kama alivyofanya Mw.J.K Nyeree wakati wa enzi za uhai wake.

Amesema kwa Mwalimu Nyerere alitumia elimu yake pamoja na ujuzi wake katika kupigania taifa pamoja na watanzania kwa ujumla na kuweza kufanikisha kutokana na kujitoa pamoja na kuwatumikia wananchi bila ya kujali huwezo wao.

Wamewataka watanzania ili kuweza kumuenzi Mwalimu ni lazima kuweza kuenzi matendo yake yote aliyoyafanya kama kupinga rushwa na unyanyasaji, huku akiwataka vijana hao  kuchakua jukumu la kuweza kutetea maslai ya nchi hii.

“Kama vijana  kupitia aliyoyaenzi Mwalimu ni lazima kuungana kwa pamoja na kwa na azimio moja tu la kuweza kuleta mabadiliko ndani ya nchi yetu  kama kweli sisi vijana ni taifa la leo na sio kesho ili kuleta mabadiliko”.Amesema Paschal.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa