Tone

Tone
Home » » RATIBA YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ACP LIBERATUS BARLOW.

RATIBA YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA ALIYEKUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA ACP LIBERATUS BARLOW.



Kamati ya maandalizi ya mazishi ya
aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Msaidizi wa Polisi
Liberatus Barlow, kwa niaba ya Inspekta Jenerali wa Polisi, inapenda
kuwajulisha wananchi wote utaratibu wa mazishi utakavyokuwa kuanzia
mwili kuagwa Mkoani wa Mwanza, Dar es Salaam na kuzikwa nyumbani kwao
Mkoani Kilimanjaro.

Jumapili tarehe 14/10/2012 mwili wa Marehemu utaagwa Mkoani Mwanza.

Jumatatu tarehe 15/10/2012 mwili wa Marehemu utasafirishwa kutoka mwanza kuelekea Dar es Salaam nyumbani kwake Ukonga.

  • Jumanne tarehe 16/10/2012 mwili utaagwa nyumbani kwake
    Ukonga Jijini Dar es Salaam na baadae kusafirishwa kwenda nyumbani kwao
    Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika Jumatano tarehe
    17/10/2012.

Taarifa zitaendelea kutolewa mara kwa mara kadiri ya mipango itakavyokuwa inaratibiwa katika  kila Mkoa mwili utakapofika.

Imetolewa na:
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Polisi Makao Makuu

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa