na Jovither Kaijage, Ukerewe
IDARA
ya Afya wilayani hapa, haijapelekewa dawa na vifaa tiba kwa miezi mitano sasa
hali ambayo inasababisha huduma za afya kuendelea kuwa duni.
Kaimu
Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk. Joseph Odera, alisema hayo jana katika majumuisho ya
mafunzo ya siku tano kwa watumishi wa umma yaliyoandaliwa na Mfuko wa Bima ya
Afya (NHIF).
Alisema
mara ya mwisho idara hiyo kupokea dawa na vifaa tiba kutoka Bohari Kuu ya Dawa
(MSD), ilikuwa Mei, mwaka huu na hadi sasa hakuna kilichopelekwa.
Alisema
huduma za tiba katika wilaya hiyo, zinakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo
kupata idadi kubwa ya wagonjwa hasa wanaotoka eneo la wilaya jirani ya Bunda,
Mara na mwingiliano wa idadi kubwa ya watu wanaotafuta shughuli za uvuvi.
Naye
Ofisa Idara ya wananchama wa NHIF Kanda ya Ziwa, Gabuliel Shole, alisema
wanachama wa mfuko huo wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo kukosa dawa
na vifaa tiba, huku wakikumbana na kauli za kejeli pindi wanapokwenda kupata
huduma za tiba katika vituo vya afya na hospitali.
Alisema
katika kipindi cha siku tano, wamefanikiwa kuzifikia kata 21 za wilaya hiyo na
kutoa mafunzo ya huduma za mfuko huo kwa wanachama 812, wengi wao wakiwa
walimu.
Shole
alisema wakati wa mafunzo hayo wamekumbana na changamoto hizo zikiwemo za
kukosa huduma nzuri na maalumu inayolingana na gharama za fedha wanayokatwa
kuchangia mfuko wa NHIF.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment