Tone

Tone
Home » » Inter-ports-Games yaanza kwa kishindo!

Inter-ports-Games yaanza kwa kishindo!

 Bandari Tanga wakiingia uwanjani kabla ya kuanza kwa michezo.
 Mpira wa pete ulikuwa ni kivutio cha aina yake.
 Timu ya Bandari kwa upande wa maziwa ikiingia uwanjani.
  Goli likifungwa katika mtanange wa mpira wa pete.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akisoma hotuba yake kabla ya kufungua rasmu michezo hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Jones Macha.

======  =======  =====  ====

Inter-ports-Games yaanza kwa kishindo!
Michezo ya Bandari maarufu kama ‘inter-ports games’ imeanza rasmi katika viwanja vya CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo mashabiki wameonesha kuridhishwa na michezo ya awali ya ufunguzi huku wachezaji wakionesha vipaji vya hali yajuu katika michezo ya soka, mpira wa kikapu, pete na kuvuta kamba.

Michezo hiyo ambayo imefunguliwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba (MB),aliyefurahishwa na kuridhishwa na maandalizi yake, inategemewa kufanyika kwa muda wa siku tano kuanzia Agosti 15 katika jiji la Mwanza.

Dk. Tizeba amewaasa wachezaji kucheza kwa upendo na staha na kukumbuka kwamba michezo inajenga undugu na mshikamano na si uadui. Aidha amewakumbusha wachezaji kuendelea kushiriki katika michezo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha afya zao mara baada ya kukamilka kwa michezo hii.

Michezo ya ‘inter-ports games’ inazikutanisha bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Mwanza, Kyela, Kigoma na Makao Makuu ambapo michezo ya mpira wa miguu, kuvuta kamba, bao, riadha, kikapu na mprira wa pete itashindaniwa.
Na: Focus Mauki
Afisa Mawasiliano
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)




 Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba akikagua timu ya soka kabla ya kuanza kwa mtanange wa ufunguzi kati ya Dar es Salaam Port na Mwanza Port.
 Mchezo wa bao ambao ni maarufu kote nchini pia unashindaniwa  katika michezo hii.
 Wanaume wa shoka wa mchezo wa kuvuta kamba kutoka Dar es Salaam port wakiwania ushindi.
 Mkurugenzi wa Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Alhaj Juma Abdulrahmaan akizungumza katika ufunguzi wa michezo hiyo.
 Daktari Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Dkt. Mkunde Mlay akisaidiana na vijana wake kutoa huduma ya kwanza kwa wachezaji walioumia.
 Mpira wa kikapu ulikuwa na ushidani wa hali ya juu.
 Mashabiki wakionesha hisia zao.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa