Home » » HATIMAYE ANTONY MWANDU DIALLO ASHINDA UENYEKITI CCM MKOA WA MWANZA KWA KUMBWAGA CLEMENT GREGORY MABINA.

HATIMAYE ANTONY MWANDU DIALLO ASHINDA UENYEKITI CCM MKOA WA MWANZA KWA KUMBWAGA CLEMENT GREGORY MABINA.




Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, na mbunge wa zamani wa Jimbo la Ilemela jijini Mwanza, Anthony Mwandu Diallo, ameibuka mshindi kwa kura 611 katika wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, kisha kumgalagaza aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Clement Gregory Mabina aliyepata kura 328.

Akitangaza matokeo Waziri katika ofisi ya Waziri Mkuu uratibu,sera na bunge Mheshimiwa William Lukuvi amesema kuwa amempongeza bwana Diallo na kusema kuwa ushindi wake ulete mshakamano ndani ya chama na kujitahidi kukijenga chama cha Mapinduzi ili kizidi kuwa chama cha matumaini kwa watanzania wote.

Uchaguzi huo ulikuwa wa vuta nikute ulianza asubuhi kwa kuchagua wajumbe wa uongozi mbalimbali na wawakilishi wa Mkoa na baadae ukafuatia nafasi mbalimbali nyeti za Mkoa ambazo kuwa zaidi iliokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wana CCM wote kutoka wilaya za Mkoa Mwanza. 

Mbali na Diallo, wagombea wengine wa nafasi ya uenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, waliotangazwa na msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu na Bunge, William Lukuvi ni pamoja na Zebedayo Athumani (kura 4), Hussein Mashimba (kura15), Joseph Langula Yared (kura 30), na Mabina ambaye alipata (kura 328) wote kati ya kura zote 988 halali zilizopigwa.


Wakati wajumbe wakingoja wajumbe wenzao kutoka wilaya zingine kulitokea ajali ya basi lililobeba wajumbe wa mkutano mkuu wilaya ya Kwimba, ambapo basi lao limepata ajali na kuanguka eneo la Buhongwa wilaya ya Nyamagana, mkoani Mwanza  majira ya saa 3:30 - 4:00 asubuhi ambapo ilitajwa kuwa dereva wa chombo hicho cha usafiri amefariki dunia papo hapo na wajumbe wengine saba kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando.

Chanzo cha ajali hiyo kilitajwa kuwa basi hilo lilikuwa katika mwendo kasi na katika harakati yakulikwepa roli aina ya fuso ambalo lilikuwa likigeuza kujiweka sawa kuingia barabarani ndipo basi hilo lilipopoteza uelekeo na kulibamiza fuso na kupinduka.


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa