na Jovither Kaijage, Ukerewe
WENYEVITI
wa vitongoji na vijiji wilayani Ukerewe, Mwanza wanaodai posho ya kusimamia
Sensa ya Watu na Makazi, wamepitisha azimio la kumshitaki mahakamani mkuu wa
wilaya hiyo.
Wenyeviti
hao wa vitongoji na vijiji wapatao 256 walipitisha azimio hilo jana katika
kikao chao kilichofanyika mjini hapa.
Viongozi
hao walifikia uamuzi huo baada ya kutoridhishwa na majibu yanayotolewa na
Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Mariam Mseleche na Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya hiyo, Joseph Mkundi, ambao nao walishiriki kikao hicho.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji wa wilaya hiyo, Hussein Hassan,
alisema mbali ya azimio hilo pia wamekubaliana kususia shughuli zote za
maendeleo na kuongeza kuwa hivi sasa wanawasiliana na wanasheria, ili suala
hilo walifikishe mahakamani kwa utatauzi wa kisheria.
Katika
madai yao, kila mwenyekiti wa kitongoji anadai posho ya sh 140,000 pamoja na
posho ya madaraka ya kila mwezi ambayo hawajalipwa tangu Septemba mwaka jana
mpaka sasa.
Katika
hatua nyingine viongozi hao wa vitongoji na vijiji wametaka posho ya madaraka
kwa wenyeviti wa vitongoji iongezwe kutoka sh 5,000 ya sasa hadi sh 35,000 kwa
mwezi huku wenyeviti wa vijiji wakitaka iongezwe kutoka sh 10,000 hadi 50,000.
Katibu
Tawala wa wilaya hiyo, Mariam Mseleche, akizungumzia madai hayo alisema yapo
nje ya uwezo wake na kuaidi kuyafikisha katika mamlaka husika.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Joseph Mkundi, ameahidi kufuatilia na
kupata ukweli wa madai ya kutolipwa posho ya madaraka na kulipatia ufumbuzi.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment