Mwandishi wetu, Ukerewe
WAKAZI wa wilaya ya Ukerewe , Mwanza wameimizwa kujitokeza kutoa maoni yao katika tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya ikiwa ndio njia pekee ya kupata katiba inayokizi matakwa ya wengi.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kiruthel Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki ya Ziwa Victoria, Andrea Gulle ametoa wito huo jana mjini Nansio wilaya ya Ukerewe, Mwanza.
Ibada hiyo maalumu ilifanyika katika usharika wa Nansio ya kumuingiza kazini mkuu wa jimbo la Ukerew, mchungaji Elias Lugaganya pamoja na kuweka jiwe la msingi katika nyumba ya mtumishi wa usharika huo
Alisema waumini wa kanisa hilo pamoja na jamii kwa jumla wanatakiwa kutambua kuwa katiba ndio muongozo wa maisha yao ya kila siku na kuwataka wajitokeze na kutoa maoni yao ili baadae ipatikane katiba yenye tija kwa wengi.
Katika hatua nyingine Askofu Gulle amewataka waumini wa kanisa hilo kuepuka matendo machafu hasa ya ndoa za jinsia moja pamona na mafundisho yasiyozingati maelekezo ya kikrsto.
Akieleza zaidi alisema kanisa la KKKT linapinga vikali ndoa za jinsia moja na kuoya kuwa waumini wa kanisa hilo wanatakiwa kuwa makini na baadhi ya makanisa yanayoanzishwa sasa yenye matendo yanayekwenda kinyume na maandiko ya kitabu kitakatifu cha Biblea.
Akitoa mfano alisema hivi karibuni yameanzishwa makanisa ambayo yanaendesha ibada kwa matendo ya yasiofaa ikiwemo viongozi wa makanisa hayo kubebwa mgongoni na waumini wao huku mengine yakialalisha viongozi wake kuzini na waumini wake.
Akifafanua alisema mbali ya mafundisho hayo kuwa kinyume na kitabu kitakatifu cha Biblea pia matendo hayo yanakiuka haki za binadamu na na yanaweza kueneza magonjwa kama Ukimwi.
Hata hivyo kiongozi huyo wa kanisa la kkkt dayosisi ya mashariki ya ziwa Victoria amewataka viongozi wa kanisa hilo kuendelea kuelimisha waumini wao juu ya madhala ya matendo hayo ili kuwa na jamii yenye maadili mema na afya njema.Mwisho.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment