Home » » Mbunge wa Ilemela adai CCM ilipanga kumuua , Spika ampa siku saba kuthibitisha

Mbunge wa Ilemela adai CCM ilipanga kumuua , Spika ampa siku saba kuthibitisha


•  Spika ampa siku saba kuthibitisha

na Mwandishi wetu
MBUNGE wa Ilemela, Highness Kiwia (CHADEMA), amedai kuwa baadhi ya wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza walitaka kumuua.
Alisema anashangazwa na  serikali kulifumbia macho suala hili  licha ya taarifa zake kufikishwa mikononi mwa vyombo vya usalama.
Akichangia mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kwa mwaka 2012/2013,  Kiwia alisema mpango huo uliandaliwa siku nyingi na alipata taarifa hizo muda mrefu, akazipuuza.
Mbunge huyo alisema kuwa wafuasi wa CCM walimteka na kutaka kuitoa roho yake wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo uliofanyika jimboni kwake katika Kata ya Kirumba jijini Mwanza.
“Wafuasi hao walitaka kuniua lakini kwa kuwa mimi nimefinyangwa kwa mikono ya Mwenyezi Mungu sitaweza kufa hadi hapo Mungu atakapotaka. Kutokana na maumivu niliyoyapata nililazimika kwenda India kwa ajili ya matibabu,” alisema Kiwia.
Mbunge huyo alisema kuwa mabadiliko na maendeleo ya wana Ilemela hayawezi kuondoka kwa wafuasi wa CCM kukatisha uhai wake.
Aidha, alisema serikali imekuwa ikifumbia macho mambo ya kinyama ambayo yamejitokeza kwa baadhi ya watu kuwateka wengine na kuwafanyia vitedo vya kinyama.
Mbunge huyo alisema vitendo hivyo vinaonyesha  kuwa serikali inapanda mbegu mbaya kwa vizazi vijavyo jambo ambalo ni hatari.
Baada ya kumaliza kujadili hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu wa Bunge),  William Lukuvi aliomba  mwongozo kama tuhuma alizozitoa mbunge ndani ya Bunge kuwa wafuasi wa CCM walitaka kumuua ni za kweli na atoe ushahidi.
Naibu Spika, Job Ndugai, alimtaka mbunge huyo kutoa ushahidi wa tuhuma hizo ndani ya siku saba na Kiwia aliomba kupewa muda ili aweze kuwasilisha vielelezo likiwamo gari la mbunge wa Viti Maalumu Mariam Hewa ambalo lilikuwa katika tukio
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa