Tone

Tone
Home » » MISUNGWI WASHINDWA KUKAMILISHA MAABARA

MISUNGWI WASHINDWA KUKAMILISHA MAABARA

 LICHA ya Serikali ya Mkoa wa Mwanza kutoa muda wa ziada kwa halmashauri kumaliza ujenzi wa maabara kwenye sekondari za kata, Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi imeshindwa kutekeleza kwa wakati agizo hilo.
Hayo yalibainika jana baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kutembelea sekondari tano za Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na kukuta maabara hizo hazijakamilika licha ya baadhi ya majengo kubadilishwa matumizi yake.
Hata hivyo, hakusita kupongeza juhudi za ujenzi zilizoonekana kwenye Sekondari ya Sanjo ambayo ilikuwa tayari ina mbao za kupaua pamoja na Sh milioni 1.5 kwa ajili za kununua mabati ambapo aliagiza ofisi yake kuwaongezea kiasi cha Sh milioni 1 ili waweze kukamilisha kazi hiyo.
Akiwa wilayani hapo, Mulongo alionesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa maabara hizo huku uongozi, wakiwemo madiwani wakijitetea kuwa michango ya wananchi imekuwa ikisuasua hivyo kukwamisha zoezi hilo kukamilika kwa wakati.
Akizungumza, Mtendaji wa Kata ya Bulemeji, Julius Mayeka alisema hali ya michango ya wananchi si nzuri, huku baadhi ya viongozi wakiwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo kuwawia vigumu kwenye ukusanyaji wa michango.
Naye kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Khalid Mbitiaza alisema wananchi wameitikia mwito wa ujenzi wa maabara na wanaendelea kwa kasi kutekeleza agizo hilo, lakini si wote watakaoweza kumaliza ifikapo Desemba 30, mwaka huu kutokana na tatizo la fedha.
 Chanzo:Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa