Tone

Tone
Home » » PICHA Za Wabunge Wa CHADEMA Walijeruhiwa na Mapanga Mkoani Mwanza Tunaomba Radhi kwa Picha ambazo mtaziona hapa

PICHA Za Wabunge Wa CHADEMA Walijeruhiwa na Mapanga Mkoani Mwanza Tunaomba Radhi kwa Picha ambazo mtaziona hapa

 Awali, wabunge hao walilazwa katika Hospitali ya Rafaa Bugando lakini baadaye walisafirishwa kwa ndege kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dar es Salaam. Kwa upande wake, Waziri amelazwa Bugando.Kamanda Barlow alisema katika vurugu hizo magari matatu likiwemo la Kiwia yaliharibiwa.
 Majeraha aliyopata kichwani mh.Highness Kiwia
 Majeraha mgongoni mwa mh. Highness.




Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Mabina amekana wafuasi wake kuhusika na uvamizi huo dhidi ya wabunge hao, akidai kwamba pengine wabunge hao walikutana na wahuni au majangili wakawavamia na kuwashambulia kwani mazingira ya usiku namna hiyo huwezi kuamini kwamba CCM wamefanya shambulio hilo nakuwataka wabunge hao wahojiwe zaidi walikwenda kufanya nini maeneo hayo nyakati hizo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow alisema juzi kwamba mbali na wabunge hao, Samson Highness Kiwia wa Ilemela (kushoto) na Salvatory Machemuli wa Ukerewe (kulia) PICHANI, wengine walioshambuliwa ni pamoja na Ahmed Waziri ambaye inasemekana kuwa ni kada wa UVCCM aliyekatwa kiganja chake cha mkono wa kulia.



Wengine ni Haji Mkweda (21), ambaye alijeruhiwa mguu wa kulia, Judhith Madaraka (26), aliyechomwa kisu kwenye titi lake la kushoto na mkono wa kushoto, Ivory Mchimba (26), aliyejeruhiwa kichwani na mdomoni. Majeruhi wote ukiondoa wabunge hao na Waziri, wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Picha na Habari na Mdau Albert G.Sengo

2 comments:

Henry said...

Duh, Tanzania ina watu au wanyama. how can someone do such a thing??? haiji akilini, mnyama mwenyewe kupigwa ivyo haiji akilini ndo binadamu...! I made a promise to myself, sirudi bongo mpaka niakikishe nakuja na miguu yangu ya kuku...bcs kwa mwendo huu, hapana!

Unknown said...

Hii ni hatari kubwaa

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa