Home » » UFAULU KIDATO CHA SITA 2024 WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.1

UFAULU KIDATO CHA SITA 2024 WAONGEZEKA KWA ASILIMIA 0.1




Kufuatia baraza la mitihani nchini kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2024, divisheni ya elimu sekondari ya Manispaa ya Ilemela imefanya tathmini ya matokeo hayo.

Kupitia tathmini hiyo imebainika kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 0.1 yaani kutoka asilimia 99.9 (mwaka 2023) , hadi asilimia 100(mwaka 2024).

Aidha tathmini hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa GPA umeongezeka kwa 0.1700 kutoka 2.7728 (mwaka 2023) na kufikia 2.6028 kwa (mwaka 2024).

Tathmini hii inaonyesha kuwa kati ya wanafunzi 818 ambao wamehitimu elimu hiyo ya sekondari, wanafunzi 373 wamepata divisheni I, waliopata divisheni II ni wanafunzi 335, wanafunzi 105 wamepata divisheni III na wanafunzi watano(5) wamepata divisheni IV, huku kukiwa hakuna waliopata alama 0.

Wahitimu hao 818 wametoka katika shule 8 na kati ya shule hizo, shule 3 ni za serikali na shule 5 ni za binafsi.

Kufuatia matokeo haya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Bi Ummy Wayayu amewapongeza wanafunzi wote kwa kufaulu na kuiletea sifa manispaa ya Ilemela na kuwataka wanafunzi waliopo shule kuongeza bidii zaidi ili ufaulu uendelee kupanda.

Mwisho kabisa amewapogeza walimu wa shule hizo kwa jitihada walizoonesha na kuhakikisha wameondoa alama 0.

Ikumbukwe kadri GPA inavyokuwa ndogo ndivyo ufaulu unakuwa umepanda kutoka( 2.77728) hadi (2.60828)
 


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Mwanza Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa