Kiasi
cha shilingi Bilioni 1.39 kimetumika kukamilisha ujenzi wa miundombinu
ya elimu sekondari katika Manispaa ya Ilemela ikiwemo vyumba 59 vya
madarasa, matundu 72 ya vyoo na seti ya meza na viti 2750.
Akisoma
taarifa ya makabidhiano ya miundombinu hiyo, kwa mkuu wa mkoa wa
Mwanza, mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela, Bi Ummy Wayayu amemshukuru
Rais Samia kwa fedha hizo na kusema kuwa halmashauri ilipokea fedha
kiasi cha shilingi Bilioni 1.41 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya
elimu na kutumia shilingi bilioni 1.39 hivyo kufanikiwa kuokoa shilingi
milioni 26.64
Kufuatia taarifa hiyo, Mhe Said Mtanda ambae ni
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameupongeza uongozi wa Ilemela kwa namna ambavyo
inaendelea kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya maendeleo huku
akiweka wazi jinsi alivyovutiwa na namna ambavyo Ilemela imeweza kuokoa
shilingi Milioni 26.
" Niwapongeze Ilemela kwa usimamizi mzuri wa
miradi ya maendeleo, lakini nimevutiwa na taarifa kuwa fedha takribani
Shilingi milioni 26 zimeweza kuokolewa"
Ni msimamo wa serikali,
kuwa tunapofanya shughuli za usimamizi wa ujenzi wa miradi yoyote sio
lazima fedha iliyopangwa itumike na kuisha yote,tunaweza kuokoa fedhs
na kuitumia kwa shughuli zingine ,amesema Mhe Mtanda.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Mwl Hassan Masala amefafanua kuwa
kipindi kama hiki katika miaka ya nyuma jamii ilikuwa ikikimbizana
kuchangishana fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa kinyume na sasa
ambapo Serikali ya Rais Samia imeweza kutoa fedha na kujenga madarasa na
miundombinu mingine mingi ya elimu hivyo kuwataka wananchi kuendelea
kushirikiana katika shughuli za maendeleo.
Nae Mbunge wa Jimbo la
Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za
maendeleo ndani ya jimbo hilo ,akaendelea kusema kuwa Ilemela ya miaka
10 iliyopita sio sawa na Ilemela ya sasa kwani maendeleo yanaonekana
Katika
nyakati tofauti wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lumala ambapo
makabidhiano ya ujenzi wa vyumba vya madarasa yamefanyika, wamemshukuru
Rais Samia kwa ambavyo anaendelea kuwajali kwa kuwajengea miundombinu ya
elimu kwani inawanufaisha na kuwaboreshea mazingira ya kujifunzia hivyo
wakamuahidi kusoma kwa bidii ili wafikie malengo yao.
Home »
» ILEMELA YAKAMILISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU.
0 comments:
Post a Comment